Katika
kuendeleza kasi ya rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Dk John
Pombe Magufuli, mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA imekusudia
kuwafutia leseni wamiliki wa Radio na TV wanaokwepa kulipa ada zao
sambamba na kwa makampuni ya simu yanayoshindwa kutoa huduma bora za
mawasiliano kwa watanzania.
Hayo yameelezwa mjini Morogoro na mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya
mawasiliano nchini, TCRA, INJ.Dk Ally Yahaya Simba ambaye amewataka
wamiliki wa vyombo vya habari kuhakikisha wanalipa ada zao za leseni na
madeni mengine wanayodaiwa kabla ya Dec.30 mwaka huu, vinginevyo kuanzia
Des 31 wataanza kufungiwa kwani kwa sasa wanadai takribani shilingi
milioni 800 hao, huku akiwataka wamiliki wa mitandao ya simu za mkononi
wanaotoa huduma zao chini ya kiwango na ubora unaotakiwa kutoa huduma
nzuri kwani kwenda kinyume watakabiliwa na adhabu kali sambamba na
kuwafikisha mahakamani wote watakao toa huduma mbovu.
Nao wadau wa mawasiliano mkoani Morogoro wamewasilisha malalamiko
mbalimbali kwa mamlaka hiyo hasa kwa upande wa mitandao ya simu za
mkononi kukatà ovyo mawasiliano au kukata fedha tofauti na matumizi
pamoja na kushindwa kushughulikiwa matatizo yao kwa muda muafaka huku
wengine wakihoji matumizi ya watangazaji wasio na taaluma na weledi
wakiwemo wanaoanzisha vipindi vilivyo kinyume na maadili ya mtanzania
sambamba na usumbufu wa kutumia vingamuzi vingi tofauti katika matumizi
ya TV.
Baada ya kupokea malalamiko hayo, mkurugenzi huyo ameahidi kufanyia
kazi kwa kutoa adhabu kali kwa wale wote watakao bainika kwenda kinyume
na maagizo na sheria za mamlaka ya mawasiliano Tanzania, sambamba na
kuwa katika hatua za mwisho kununua mitambo ya kufuatilia matumizi ya
simu ili serikali itoze gharama kwa makampuni ya simu kiusahihi na
kukagua huduma za masafa kama zilivyoombwa na vyombo husika.
No comments:
Post a Comment