Waziri
wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akiongea na
wahariri wa Vyombo vya Habari(hawapo pichani) jana jijini Dar es
Salaam.Mhe Nape alivipongeza vyombo vya Habari kwa kufanya wajibu wao
katika kipindi cha uchaguzi mkuu na kuwahaidi kuwa serikali itakuwa
karibu nao sana na kuhimiza kuwa serikali ya awamu ya Tano itatunga
sheria nzuri itakayoraisisha utekelezaji wa majukumu yao.Kushoto kwake
ni Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Bw.Absalom Kibanda.
Mwenyekiti
wa Jukwaa la wahariri Bw.Absalom Kibanda akiwahimiza wahariri wa
vyombo vya Habari(hawapo pichani) kuhusu kutenda wajibu wao wakati wote
wanapofanya kazi zao kwani uhuru waendani na wajibu jana jijini Dar es
Salaam.kulia kwake ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
Mhe.Nape Nnauye na wa mwisho ni Kaimu mkurugenzi mkuu Idara ya
Habari-MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa.
Mhariri
mkuu wa Gazeti la The Guardian Bw.Jesse Kwayu akichangia hoja wakati
wakati wa kikao kati ya wahariri wa vyombo vya habari na Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe Nape Nnauye.Bw Kwayu alimsihi Mhe
Nape kuzidi kuwa karibu na waandishi na pia zitungwe sheria
zitakazowawezesha waandishi wa habari kupata habari kwa urahisi na
kufanya kazi yao ya kuhabarisha jamii.
Mhariri
Mtendaji wa magazeti ya Jamhuri Media Ltd Bw.Deodatus Balile akichangia
hoja katika kikao kati ya wahariri wa vyombo vya habari na Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.
Mhariri
wa Gazeti la the Citizen Bw Peter Nyanje akichangia jambo wakati wa
kikao kati ya wahariri wa vyombo vya habari na Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.Picha na Daudi Manongi-Wizara ya habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo(WHUSM).
Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Mh.Nnape Nnauye akiwa katika picha ya
pamoja na na baadhi ya Wakuu wa Idara ya Habari Maelezo na Wahariri
kutoka vyombo mbalimbali vya habari mapema jana,alipokutana nao na
kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili tasnia hiyo,mkutano huo
umefanyika kwenye moja ya ukumbi ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh.Nnape Nnauye akiwa katika picha ya
pamoja na na baadhi ya Wakuu wa Idara ya Habari Maelezo na Wahariri
kutoka vyombo mbalimbali vya habari.
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh.Nnape Nnauye akizungumza na Wahariri wa
vyombo vya habari (hawapo pichani),mapema jana jijini Dar,kwenye mkutano
uliohusu kujadili mambo mbalimbali zikiwemo changamoto zinazoikabili
tasnia ya habari hapa nchini.Pichani kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la
Wahariri Absalom Kibanda na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari
MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa .
Kaimu Mkurugenzi Idara ya
Habari MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa akiwakaribisha Wahariri wa vyombo vya
habari (hawapo pichani),mapema jana jijini Dar,kwenye mkutano
ulioitishwa na Waziri Nape kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali
yanayoikabili tasnia ya habari hapa nchini.Pichani kati ni Waziri
Mh.Nape pamoja na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda.
Mwenyekiti wa Jukwaa la
Wahariri Absalom Kibanda akitoa muongozo kwa Wahariri wa Vyombo vya
habari (hawapo nchini) kuhusina na mkutano wao ulioitishwa na Waziri
Nape kujadili mambo mbalimbali na changamoto zinazoikabili tasnia hiyo
kwa ujumla.
Baadhi ya Wahariri wa
vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano huo wakifuatilia mambo
mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa ukumbini humo.
Mmoja wa Wahariri Kurwa
Kaledia kutoka New Habari House akiomba ufafanuzi wa jambo kwa Mh Waziri
Nape huku baadhi ya wahariri wakifuatilia kwa makini.
Mmoja wa Wahariri Grace Hoka akifafanua jambo kwenye mkutano huo.
Baadhi ya Wahariri wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo.
Baadhi ya Wahariri juu pichani wakishiriki kuchangia mambo mbalimbali kwenye mkutano huo.
Mmoja wa Wahariri akifafanua jambo kwenye mkutano huo.
Baadhi ya Wadau wakubwa wa habari pia walikuwepo kwenye mkutano huo.(PICHA NA MICHUZI JR).
No comments:
Post a Comment