TTCL

EQUITY

Sunday, January 10, 2016

Serikali ya ahidi kuendelea kutatua kero za wasanii

PIX1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (mwenye shati la batiki) akizungumza na wajumbe wa Kamati ya wasanii wa Muziki inayofuatilia suala la malipo ya mrabaha kutokana na kazi zao Jijini Dar es Salaam.

PIX2a
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwezeshaji Mhe. Charles Mwijage akizungumza na wajumbe wa Kamati ya wasanii wa Muziki inayofuatilia suala la malipo ya mrabaha kutoka kwa vyombo vya habari na miito ya simu. Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye na kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mungereza jana jijini Dar es Salaam.
PIX2b
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya ambaye pia ni Kiongozi wa Kamati ya wasanii wa muziki Bw. Nickson Simon kwa jina la kisanii Nikki wa Pili akiwasilisha hoja za kwa niaba ya wasanii wenzake wakati wa kikao baina yao na waheshimiwa Mawaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja Mhe. Nape Moses Nnauye na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwezeshaji Mhe. Charles Mwijage jana jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sana Bibi. Leah Kihimbi na kushoto ni msaanii Ditto.

PIX3
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya ambaye pia mjumbe wa Kamati ya wasanii wa muziki akichangia mada wakati wa kikao baina yao na waheshimiwa Mawaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja Mhe. Nape Moses Nnauye na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwezeshaji Mhe. Charles Mwijage jana jijini Dar es Salaam.

PIX4
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na msanii mkongwe wa muziki wa injili Bw. Cosmas Kidumule mara baada ya kumaliza kikao na Kamati ya wasanii jana jijini Dar es Salaam.

PIX5
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (aliyevaa batiki) na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwezeshaji Mhe. Charles Mwijage wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii mara baada ya kumaliza kikao na Kamati ya wasanii jana jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment