Kocha
mpya wa Real Madrid, Zinedine Zidane ameanza vyema kazi ya kuiongoza
klabu hiyo kwa kupata ushindi wa goli 5 kwa bila dhidi ya Deportivo La
Coruna katika mchezo wa Ligi Kuu ya Hispania uliochezwa kwenye uwanja wa
Santiago Bernabeu.
Magoli
ya Real Madrid katika mchezo huo yalifungwa na Karim Benzema dk. 15 na
90 na Gareth Bale (pichani) aliyefunga hat trick dk. 23, 49 na 63.
Baada
ya kumalizika kwa mchezo huo Zidane alisema mchezo huo umekuwa mzuri
kwake na kila jambo ambalo alikuwa amelipanga limetokea kama jinsi
alivyokuwa akitarajia na amependezwa na hali ya mchezo ilivyokuwa.
“Nimependa
hali ya mchezo kwa ujumla, tumeshinda goli 5 haikuwa rahisi kwa timu
kama La Coruna nina furaha sana na mchezo, nimependa hali ya mchezo, kwa
waliocheza na ambao hawakucheza,” alisema Zidane.
Aliongeza
kuwa baada ya matokeo hayo mazuri kutawapa nafasi ya kufanya mazoezi
zaidi ili wazidi kuwa bora kwa michezo iliyopo mbele yao na anaamini
watafanikiwa kwa michezo mingine inayowakabili.
No comments:
Post a Comment