Uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja barani Afrika ulipungua mwaka jana kwa asilimia 31 ambayo ni sawa na dola bilioni 38.
Katibu Mkuu wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo, UNCTAD, Dkt. Mukhisa Kituyi.
Hiyo
ni kwa mujibu wa ripoti ya awali ya makadirio ya uwekezaji mwaka 2015
kimataifa iliyotolewa na Kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na
maendeleo, UNCTAD, mwezi huu wa Januari ambapo kwa mujibu wa ripoti
hiyo, mataifa mengi ya Afrika yameshuhudia kushuka kwa uwekezaji wa
kigeni hususani yale ya Kusini mwa Sahara.
Katibu Mkuu wa UNCTAD, Dkt. Mukhisa Kituyi ametaja sababu za mataifa
ya Afrika kusini mwa Sahara kukumbwa na hali hiyo inatoka na mataifa
makubwa kuanza kujitoa katika nchi walizokuwa wanawekeza katika rasimali
ya mafuta.
Mataifa ya Afrika yaliyoko kaskazini kama vile Misri yalishuhudia
kuongezeka kwa uwekezaji huku Marekani ndio kidedea katika nchi kumi
zilizopata uwekezaji wa juu zaidi, nyingine ni China, Uingereza na
Ufaransa ikichukua nafasi ya kumi.
No comments:
Post a Comment