TTCL

EQUITY

Sunday, November 15, 2015

Ukawa utatoa mgombea Uspika makini

Mwenyekiti wa Chadema na Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, Freeman Mbowe
Mwenyekiti wa Chadema na Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, Freeman Mbowea.

MBUNGE mteule wa jimbo la Hai na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Freeman Mbowe (Chadema) amesema mchakato wa kumpata spika wa Bunge unaendelea ndani ya umoja huo.
Mbali na hilo amesema siyo dhambi kumpata spika ambaye hatokani na wabunge na asiye kuwa na chama chochote cha siasa.
Mbowe alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza waandishi wa habari juu ya mchakato wa kumpata Spika wa Bunge la kumi na Moja.
Mbowe alisema mchakato wa uspika ndani ya umoja wao unaendelea na watakapo maliza wataweka adharani majina ya watu waliochomoza.
Akizungumzia hoja ya Spika kuwa mbunge au la alisema inafaa zaidi Spika kutokuwa mbunge na asiye kuwa na chama chochote cha siasa.
Amesema kuwa mbunge siyo sifa ya kuwa unakubalika kwani kuna watu ambao wamekuja bungeni lakini hawakuchaguliwa na wananchi.
“Ninyi waandishi mnajua kuwa uchaguzi ulivyokuwa wapo watu ambao wamekuja bunge bila kushinda na wengine wametangazwa bila hata kupigiwa kura”. Alisema
“Inafaa zaidi kama angepatikana spika ambaye hatokani na chama chochote cha siasa ili kuweza kuondokana na ushabiki wa kulinda maslahi ya chama fulani.
“Wapo watu wengi ambao siyo wabunge lakini wanaweza kuendesha vyema bunge jambo ambalo akipatikana spika toka nje ya bunge anaweza kuendesha bunge vizuri” alisema Mbowe.
Kauli ya Mbowe imetokana na Mbunge mteule wa jimbo la Mtera Livingston Lusinde (CCM) aliyenukuliwa akisema spika lazima awe mbunge.
Lusinde akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa mtu yoyote ambaye anatoka nje ya hataweza kumpigia kura.
Kwa upande wake Mbunge mteule wa jimbo la Kisarawe Sulemani Jafo (CCM) alisema spika ambaye atapatikana ni lazima alisimamie vizuri Bunge.
Amesema wananchi wengi wana matarajio makubwa na bunge kwa maana ya dhana ya mabadiliko.
Mbali na hilo alisema wabunge wanatakiwa kulitumia Bunge kwa lengo la kuisimamia selikari kwa lengo la kutetea maslahi mapana ya watanzania wote bila kujali itikadi za vyama.
“Nataka kuwaambia wabunge wenzangu hususani vijana wahakikishe wanafanya kazi ya kuisimamia serikali bila kujali itikadi za vyama vyao na wala kupingana kama vile wanakomoana.
“Pale penye ukweli ni vyema wabunge wote tukakubaliana kwa nia moja kwa lengo la maslahi mapana ya watanzania wote,” amesema Jafo.

No comments:

Post a Comment