Hawa ni moja kati aya vijana walio onesha umahiri wa kujieleza na kuelezea mada zilizo kuwa na tija kwa jamii, katika shindano la IYF English Speech, na kuweza kuwa washindi ambapo walijinyakulia simu na kamera za kisasa.
Vijana ndiyo msingi wa maendeleo ya taifa letu, na ni muhimu vijana wakatambua hilo kwa kutimiza wajibu wao kwa jamii inayowazunguka. maneno hayo yaliwahi kusemwa na Dkt. Fenella Mukangara Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, kwa mara ya kwanza alipo alikwa katika ufunguzi wa kambi ya mafunzo ya vijana IYF yaliyo fanyika August 9 2012 Jijini Dr es salaam. Tanzania ni nchi yenye vijana wengi wasio na ajira lakini wenye vipaji, huku baadhi yao wakiwa hawana ujuzi na kutojua lugha za kimataifa.
IYF (International Youth Fellowship) ni shirika la vijana linalofanya kazi kwakushirikiana na wizara ya habari, vijana, utamaduni na michezo, na yenye makao makuu yake nchini korea ya kusini, lakini ikiwa zaidi ya nchi 80 duniani.
Taasisi hii imekuwa ikiwaweka vijana pamoja kwa kuandaa kambi ikiwa lengo ni kutoa mafunzo mbalimbali kwa hususa ni Lugha (kichina, kikorea, kiingereza, kitailand), burudani na michezo (kuimba, kucheza, kutumia vifaa vya muziki), saana ya ngumi (Taekwo ndo), elimu ya dini, michezo na elimu ya ufahamu, mashindano ya uwasilishi wa mada mbalimbali kwa lugha ya kiingereza (public speaking).
IYF ambayo imezoeleka kuitwa English Camp Msimu huu 2014 iliandaa, Elimu na
michezo ya Ufahamu, lugha, elimu kuhusu dini, na uwasilishaji wa mada kwa
kingereza, ambapo mwaka huu mshindi wa kwanza aliibuka msichana, kwakutoa mada
nzito iliyohusisha siasa na maendeleo ya vijana na mshindi wa pili alikuwa Bwa.
Elvis Eliphaz aliyewatoa wanaume kimasomaso.Bi. Rogathe Manasseh Loakaki
anayesoma kidato cha Tano shule ya Cornestone High School akitokea Sanawari ni
binti pekee aliyeonesha kujiamini, akizungumza kwa vitendo huku akitumia mifano
mbalimbali na kufanya umati wa watu kuwa makini mkusikiliza, zaidi aliibua
hisia za watu pale alipotajwa kuwa mshindi wa kwanza na kuwafanya wasichana
kuona kuwa wanaweza, kilichonipa ushindi ni Mungu, wala sio kwa akili zangu
pekee, kujiamini na kushirikisha wengine kulinipa uwezo zaidi.
Aidha malengo ya IYF ni kuwaweka vija wa kitaifa na kimataifa pamoja na kuleta
ushirikiano kati yao, ili kuleta nguvu ya ufikiri pamoja kama leo hapa tumekuwa
na vijana wa Arusha, wengine wanatoka nje ya Arusha na wengine kutoka nje ya
nchi, kwa kusanyiko letu tunapata ufahamu tofauti, pamoja na kumjua Mungu. Ni
Oresto Adam Mwanachama na kiongozi wa IYF Ambapo alikuwa akizungumza nami.
Program hii hufanyika mara moja kwa mwaka kwa kila mkoa, na hadi sasa
imefanyika Mbeya, Arusha na Dar es salaam, ambapo lengo ni kuweza kuifikia
Tanzania nzima na dunia kwa ujumla. Vilevile kuna program hii ya World Camp
ambapo hufanyika Dar es salaam na kukusanya vijana kutoka wilaya, na mikoa
tofauti , pamoja na wengine kutoka nje ya nchi.
Pia kutoka na kuwepo kwa program nyingi pia tunayo ingine ya kimataifa hii
inatwa Good News Cops (GNC) hii inatoa fursa kwa vijana kwenda kujifunza na
kufundisha mataifa mengine, na kushiriki katika kujifunza namna wengine walivyo
piga hatua, na msimu wapili wa GNC utafanyika wiki ijayo katika viwanja vya
Mbezi Beach Jijini Dar es salaam 27 Oct. 2014
No comments:
Post a Comment