Serikali imesema ili kukabiliana na tatizo la
ajira kwa wahitimu wa elimu ya juu ambao wengi wao ni vijana imeandaa
mpango maalumu ikiwa ni pamoja na kuimarisha wakala wa huduma za ajira
nchini Tanzania (TAESA).
Naibu waziri wa Nchi Bunge Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Anthony Mavunde.
Hayo
yamesemwa leo Bunge na Naibu waziri wa Nchi Bunge Kazi, Ajira, Vijana
na Watu wenye Ulemavu Mhe. Anthony Mavunde ambapo amesema wakala hutakiwa kutimiza jukumu lake ipasavyo la kuwaunganisha watafuta kazi na
waajiri wa ndani na nje ya nchi.
Aidha Mhe Mavunde ameongeza kuwa mpango mwingine ni pamoja na kuandaa
mkakati wa kukuza ujuzi nchini ambao utaanza kutekelezwa mwaka ujao wa
fedha 2016/2017 ambao utajikita zaidi katika kuwezesha mafunzo ya
vitendo mahali pa kazi.
Mhe. Mavunde alikuwa anajibu swali la mbunge wa Vwawa Mhe Japhet
Ngailonga Asunga ambaye alitaka kujua mpango wa serikali katika kujua
idadi ya wahitimu wa elimu waliokosa ajira na mpango wa kuwawezesha
kupunguza tatizo la ajira kwa wanaomaliza elimu ya juu.
No comments:
Post a Comment