Mkutano wa pili wa Bunge la 11 umeanza hii leo
mjini Dodoma pamoja na shughuli nyingine wabunge watajadili mpango wa
maendeleo awamu ya pili na hotuba aliyoitoa Rais Dkt. Magufuli huku
mjadala wa kuhusu hali ya kisiasa Zanzibar ukitarajiwa kuibuka.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai
Mkutano
huo umeanza kwa kiapo cha uaminifu kwa wabunge 11 ambao wamechaguliwa
na wengine kuteuliwa na Rais pamoja na kipindi cha maswali na majibu kwa
wizara tofauti za serikali.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma kuhusu ratiba ya
mkutano huo wa bunge mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano Bungeni
Owen Mwandumbya amesema mkutano huo ulioanza utamalizika Februari 05
mwaka huu.
Aidha mkuu huyo wa kitengo cha habari ameongeza kuwa katika mkutano
huo jumla ya maswali ya msingi ya kawaida 125 yanategemewa kuulizwa na
kujibiwa huku maswali ya msingi 16 yakielekezwa kwa Waziri Mkuu.
Ameongeza kuwa shughuli zitakazoendeshwa leo ni pamoja na uchaguzi wa
wenyeviti watatu wa bunge na ambapo juzi kamati ya uongozi ilipendekeza
majina ya wabunge watatu ambao ni Najma Giga, Andrew Chenge na Marry
Mwanjelwa kuwania uenyekiti huo.
No comments:
Post a Comment