Serikali imetakiwa kuheshimu haki ya kikatiba ya
kuwapa wananchi habari na taarifa muhimu zinazowahusu bila ya kujali
gharama za taarifa hizo kwa kuwa ni jukumu lake kufanya hivyo.
Mkurugenzi wa Uwezeshashi na Uwajibikaji wa LHRC, Bi. Imelda Lulu Urio
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na kituo cha sheria na haki za
binadamu kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi wake Bi. Imelda Urio na kuongeza
kuwa kusitishwa baadhi ya matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya bunge
kwa kisingizio cha gharama ni kitendo cha makusudi kwa kuwanyima
wananchi taarifa muhimu toka kwa wawakilishi wao ambao ni wabunge.
Bi Imelda Urio ameongeza kuwa muhimili wa bunge na viongozi wake
lazima wafanye kazi kiueledi na kuzuia mianya ya kuingiliwa na mihimili
mingine hususani serikali.
Aidha LHRC imelaani vikali kitengo cha kuzalilishwa kwa wabunge kwa kutolewa bungeni na mbwa wa jeshi la polisi.
Kwa upande wa kaimu mkurugenzi wa utetezi na maboresho Bi. Anna Henga
yeye amesema kuwa haki yoyote haina gharama na ni jukumu la serikali
kulipia gharama hizo
No comments:
Post a Comment