TTCL

EQUITY

Friday, January 29, 2016

Mikoa tisa yakabiliwa na Uhaba wa Madaktari bingwa

Serikali imesema imebaini mikoa tisa nchini Tanzania inakabiliwa na uhaba mkubwa wa Madaktari bingwa hali inayowafanya wananchi wa maeneo hayo wakose huduma bora za kiafya katika mikoa yao.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
Akiongea leo Bungeni Mjini Dodoma Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na kusema kuwa serikali inachukua za haraka za kuweza kuwasambaza madaktari hao katika mikoa hiyo.

Aidha Mhe. Ummy amesema kuwa Mpango wa serikali kwa sasa ni kuwapangua madkatari bingwa wote na kuwasambaza katika mikoa yote nchini ili Wananchi hususani wanawake waweze kupata huduma sawa na mikoa mingine ikiwemo Dar es Salaam.

Mhe Ummy aliitaja mikoa yenye uhaba huo mkubwa wa Madaktari bingwa ni pamoja Tabora, Simiyu, Katavi, Geita Shinyanga, Rukwa pamoja na Singida hivyo kuwataka wananchi wa mikoa hiyo kuwa watulivu wakati tatizo lao linashughulikiwa.

No comments:

Post a Comment