KATIKA kutambua na kuheshimu mchango wa straika, Mbwana Samatta kwa
kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa Wachezaji Wanaocheza Ndani,
uongozi wa Dar Live kwa kushirikiana na viongozi wa Wilaya ya Temeke
umeandaa sherehe ya kumpongeza staa huyo.
Sherehe hiyo itafanyika Jumanne, Januari 12, 2016 kwenye Uwanja wa
Burudani wa Dar Live uliyopo Mbagala-Zakheem kuanzia mida ya 12:00 jioni
kwa kiingilio kiduchu cha Tshs 5,000/=.
Samatta juzi aliandikisha rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza Ukanda wa
Afrika Mashariki na Kati kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika,
alipowabwaga Robert Kidiaba (DR Congo) na Baghdad Bounedjah (Algeria).
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye (kushoto mwenye tuzo) akiwa na Mbwana Samatta.
Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo ameliambia Championi Jumatatu kuwa
wameratibu sherehe hiyo kwa kuwa Samatta ni ‘mtoto wa nyumbani’ ambako
alizaliwa, kukulia na kusomea Mbagala, hivyo kulikuwa na kila sababu ya
kumpongeza kwa heshima aliyowaletea.
“Tulikuwa na kila sababu ya kumuandalia sherehe. Amezaliwa, amekulia,
amesomea, amechezea na familia yake yote iko Mbagala, hivyo lazima
tumthamini. Lakini pia mashabiki watapa nafasi ya kupiga na tuzo hiyo
pamoja na yeye,” alisema Mbizo.
Aliongeza sherehe hiyo itanogeshwa kwa burudani kutoka kwa Juma
Nature, Bendi ya Twanga Pepeta, Msaga Sumu pamoja na Khalid Chokoraa
ambaye atamtungia single yake ‘special’ kumpongeza kwa tuzo hiyo.
Pamoja na yote, pia viongozi wa Simba na Africa Lyon wamealikwa kwa
mchango wao ambako Samatta alipata kuchezea kabla ya kutimkia Mazembe
ambako ametwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika mbali na tuzo binafsi.
“Naomba watu wajitokeze kwa wingi kuonesha sote tuko pamoja na safari yake ya soka,” aliongeza Mbizo
Mwanasoka
Bora wa Afrika, Mtanzania, Mbwana Samatta akikatisha katika jiji la
Dar leo kuanzia Hoteli ya Hyatt Regency Kempinsk mpaka Escape One akiwa
katika gari la waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape
Nnauye.
…Akiendelea kuwasalimia wakazi wa jiji la Dar.
Madereva bodaboda walikuwa kivutio wakimsindikiza Samatta.
…Akiendelea kuwasalimia wananchi mbalimbali.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akiongea na wanahabari.
Nape Nnauye akiongozana na Mbwana Samatta kuingia Ukumbi wa Escape One Mikocheni jijini Dar.
Samatta akiwa na marafiki zake katika Ukumbi wa Escape One.
Mchezaji Bora Afrika, Mbwana Samatta leo
alizunguuka mitaa ya jiji la Dar kuanzia Hoteli ya Hyatt Regency
Kempinsk kupitia samora, shule ya uhuru pale karume msafara ukapinda
kawawa road mpaka Morocco ulipopinda tena Alli Hassan Mwinyi, mpaka njia
panda ya Kawe Pale Lugalo na kuelekea Old Bagamoyo mpaka Escape One
ambapo kulikuwa na hafla fupi ya kumpongeza.
No comments:
Post a Comment