TTCL

EQUITY

Tuesday, January 26, 2016

TAKUKURU kukamilisha uchunguzi kesi za ufisadi

Taasisi ya kuzuia na kupambana rushwa nchini (TAKUKURU), imesema kuwa inashughulikia kukamilisha uchunguzi wa kesi 36 za ufisadi na Rushwa kubwa ambazo zimeliingizia taifa hasara ya matrilioni ya shilingi.
 
 Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Takukuru Kamishna Valentino Mlowola 
 
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna Valentino Mlowola amesema kati ya kesi hizo kubwa 36 kesi 4 tayari zimefikia hatua ya kuombewa kibali kwa mkurugenzi wa mashtaka ili watuhumiwa wapelekwe mahakamani.

Kamishna Mlowola amezitaja kesi hizo kuwa zinahusu makampuni ya Lake Oil kwa udanganyifu katika biashara na kuikosesha serikali mapato ya billion 8.5, kesi ya shirika hodhi la reli nchini (RAHCO), kwa udanyanjifu katika kumpata mzabuni kwenye ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge).

Mlowola ameongeza kuwa kesi nyingine ni inayohusu shirika la reli nchini TRL juu ya ukiukwaji wa sheria ya manunuzi katika ununuzi wa mabehewa 25, huku akitoa onyo kwa watumishi wote wa umma kujiepusha na rushwa na kusema kuwa wahusika wote watashughulikiwa haraka.

No comments:

Post a Comment