Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akihojiwa na mtangazaji mashuhuri wa Azam TV Taji Liundi muda mfupi kabla ya kuzindua filamu mpya ya Home Coming kwenye ukumbi wa Century Cinema ,Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Wadau wa Sanaa na Utamaduni wakisubiri kushuhudia uzinduzi wa filamu mpya ya Home Coming.
Mmoja wa washiriki wa Filamu hiyo ya Home Coming ,Susan Lewis maarufu kama Natasha
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akihojiwa muda mfupi kabla ya kuzindua Cinema ya Home Coming.
Muigizaji mkuu wa filamu ya Home Coming Daniel Kijo (kushoto) akisalimana na mgeni rasmi katika uzinduzi wa filamu hiyo Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye mara baada ya uzinduzi wa filamu hiyo kufanyika kwenye ukumbi wa Century Cinema, Mlimani City jijini Dar es Salaam.
KAMPUNI Alkemist Media
inayojishughulisha na uandaaji wa filamu nchini, usiku wa kuamkia leo
ilizindua filamu mpya inayokwenda kwa jina la Homecoming.
Filamu hiyo iliyochezwa kwa mrengo wa
kuelimisha juu ya masuala ya kutokomeza ufisadi mbalimbali, ilizinduliwa
na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, ndani
ya ukumbi wa kuonyeshea sinema uliopo katika jengo la Mlimani City
jijini Dar es Salaam.
Akizungumza muda mfupi kabla ya uzinduzi
huo kufanyika Nape alisema kuwa anawashukuru waandaaji wa filamu hiyo
kwa kumpatia fursa ya pekee kwa ajili ya kuizindua filamu hiyo ikiwa ni
moja ya mwendelezo wa kuthamini kazi za wasanii mbalimbali hapa nchini.
“Nimefarijika sana kuona leo
tumekusanyika kwenye ukumbi huu kwa ajili ya kuzindua filamu ya
Kitanzania, hivyo niwapongeze wamiliki wa ukumbi huu kwa kuruhusu
kuonyeshwa kwa filamu hii hapa, najua ni mwanzo na itakuwa faraja zaidi
siku nyingine nikija hapa nikute filamu zetu zikionyeshwa maana najua
huwa ni adimu mno kuona sehemu kama hii watu wameketi kuangalia filamu
zetu..
“Kufanya hivi mimi nina imani kuwa ni
njia mojawapo ya kukuza soko letu ambalo tunajitahidi kupambana ili
tuweze kutokomeza wizi huku tukinyanyua ajira kwenye sanaa hii,” alisema
Nape.
No comments:
Post a Comment