Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akiongea na Mchezaji wa Timu ya TP Mazembe Mbwana Samatta (kulia) leo kwenye ofisi za wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
Mbwana Samatta(wa kwanza kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Mhe. Nape Nnauye (katikati) akiongea na waandishi wa Habari wakati aakimkaribisha Samatta kwenye ofisi za wizara yake.
SERIKALI imesema ipo bega kwa bega na mshambuliaji nyota wa Taifa Stars, Mbwana Samatta kokote aendako.
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye amemuambia Samatta leo
mbele ya waandishi wa habari kwamba Serikali itamuunga mkono kokote
aendako.
“Tuko na wewe pamoja kokote
uendako, pia ninakupongeza kwa kuwa sehemu ya changamoto kwa wengine
kutokana na mafanikio uliyofikia,” alisema Nape.
Samatta ameishakubaliana na
klabu ya Genk ya Ubeligiji na sasa limebaki suala la Genk kumalizana na
TP Mazembe ili mwezi Januari shughuli za uhamisho zifanyike.
Samatta alitembelea ofisi
za Wizara wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na kusema alifika hapo
kwa ajili ya kupata baraka kabla ya kwenda kokote.
“Nimekuja kupata baraka,
baraka za wazazi ni jambo muhimu sana kwa mtoto, ndiyo maana nipo hapa,”
alisema Samatta ambaye alielezea kuhusiana na mkataba wa Genk.
“Suala la kusaini bado, ila
makubaliano yote yako safi. Nasubiri wao wamalizane na TP Mazembe baada
ya hapo mambo mengine yatafuatia,” alisema Samatta.
No comments:
Post a Comment