TTCL

EQUITY

Wednesday, December 30, 2015

Iran wachokoza Marekani

In this Thursday, Dec. 24, 2015 photo released by the U.S. Navy, guided-missile destroyer USS Bulkeley participates in a replenishment-at-sea with fleet replenishment oiler USNS John Lenthall in the Gulf of Oman. Iranian naval vessels conducted rocket tests last week near the USS Harry S. Truman aircraft carrier, the USS Bulkeley destroyer and a French frigate, the FS Provence, and commercial traffic passing through the Strait of Hormuz, the American military said Wednesday, Dec. 30, 2015 causing new tension between the two nations after a landmark nuclear deal. (Mass Communication Specialist 2nd Class M. J. Lieberknecht/ U.S. Navy via AP) MANDATORY CREDIT
Manuari za Marekani

Iran ilizua taharuki miongoni mwa wanajeshi wa Marekani ilipofytua makombora yake karibu na meli za kubeba mizigo na manuari za kivita ya Marekani katika bahari ya Hormuz leo.
Majaribio hayo ya makombora yake yanatarajiwa kuibua vuta ni kuvute baina ya mataifa hayo mawili miezi michache tu baada ya kutia saini makubaliano ya kinyuklia.
Iran ilifyatua makombora kadhaa takriban kilomita moja tu kutoka kwa manuari 2 za kijeshi za Marekani na Ufaransa msemaji wa jeshi la Marekani Kyle Raines alisema.

In this Friday, Dec. 25, 2015 photo released by the U.S. Navy, the aircraft carrier USS Harry S. Truman navigates the Gulf of Oman. Iranian naval vessels conducted rocket tests last week near the USS Harry S. Truman aircraft carrier, the USS Bulkeley destroyer and a French frigate, the FS Provence, and commercial traffic passing through the Strait of Hormuz, the American military said Wednesday, Dec. 30, 2015 causing new tension between the two nations after a landmark nuclear deal. (Mass Communication Specialist 3rd Class J. M. Tolbert/ U.S. Navy via AP) MANDATORY CREDIT
”Makombora hayo yalizua taharuki kubwa kwa majeshi yetu yaliyokuwa huko’ aliongezea kusema bwana Raines.
Bahari ya Hormuz ni eneo kati ya Iran na Oman inayotumika na takriban theluthi moja ya meli zinazofanikisha biashara ya mafuta kote duniani. Hormuz ni njia muhimu inayotumika na manuari za kijeshi zinazotekeleza mashambulizi dhidi ya kundi la Islamic State.
Mwaka wa 2012 Iran ilitishia kufunga kiunganishi hicho muhimu cha mkono wa bahari yenye upana wa takriban kilomita 33.
Serikali ya Iran haijajibu shtuma hizo wala vyombo vya habari nchini humo havijaripotti kisa hicho. Hata hivyo majeshi ya Iran yalitoa ilani ya dakika 23 pekee ya kufyatua makombora yake. Manuari hiyo ya kijeshi ya Marekani ni sehemu ya kikosi cha wanamaji cha 5ft Fleet kinachokita kambi katika bahari ya Bahrain.
Iran ilitia sahihi mkataba wa kutoendeleza jitihada zake za kitonaradi na imekubali kuvunjilia mbali mpango wake wa nyuklia iliiruhusiwe kuuza mafuta yake katika soko la dunia mbali na kuondolewa vikwazo dhidi yake.
Bahari ya Hormuz ndio iliyokuwa uwanja wa vita baina ya Iran na Marekani mwaka wa 1988.
Wkati huo Marekani iliharibu Manuari 6 za kijeshi za Iran mbali na kuharibu mitambo yake ya kuchimba mafuta baharini.
Mwaka wa 1988, manuari ya kijeshi ya Marekani USS Vincennes iliyokuwa katika bahari hiyo hiyo ya Hormuz iliilipua ndege ya abiria ya Iran iliyokuwa ikielekea Dubai na kuwaua abiria wote 290.

No comments:

Post a Comment