TTCL

EQUITY

Wednesday, December 30, 2015

Waandishi wa habari 110 wauawa duniani mwaka 2015

Jumla ya waandishi wa habari 110, waliuawa duniani kote katika kipindi cha mwaka 2015, hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la maripota wasio na mipaka (RSF) .

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya RSF waandishi wa habari 67 waliuawa wakati wakitekeleza wajibu wao wa kazi katika kipindi cha mwaka huu, na wengine 43 waliuawa katika mazingira ambayo hayajaeleweka.
Waandishi wengine wa habari 27 wasio na taaluma kamili ya uandishi wa habari na wafanyakazi wengine 7 kutoka katika vyombo vya habari nao pia waliuawa.
Hali hii inaashiria kuwa waandishi wa habari wako katika hatari ya kupoteza maisha wanapokuwa wanatekeleza wajibu wao wa kazi kutokana na matukio ya kukamatwa na kufanywa mateka na makundi ya itikadi kali kama vile kundi la dola la kiisilamu .
Ripoti hiyo inazidi kutoa mwanga juu ya kuongezeka kwa matukio ya mauaji dhidi ya waandishi wa habari yanayofanywa na makundi yasiyokuwa na mahusiano na serikali kama vile makundi ya itikadi kali mfano kundi la Dola la Kiisilamu.
"Kuna umuhimu sasa wa kuandaliwa utaratibu wa kuwa na sheria ya kimataifa itakayowalinda waandishi wa habari" alisema Christophe Deloire ambaye ni katibu mkuu wa shirika la maripota wasio na mipaka.
Idadi ya waandishi wa habari 110 waliouawa mwaka huu inaashiria kuwa kuna haja ya kuchukua hatua za haraka za kukabiliana na vitendo hivyo. Mwakilishi maalumu kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atakaye shughulikia kulindwa kwa waandishi wa habari wanapokuwa wanatekeleza wajibu wao anapaswa ateuliwe bila kuchelewa," ameongeza kusema Deloire.

No comments:

Post a Comment