Wizara ya Nishati na Madini
imewaagiza watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha
uzalishaji wa umeme katika Mradi wa Kinyerezi I na Kinyerezi II
unakamilika ifikapo mwezi Februari 2016 na kuanza kufanya uzalishaji
ilikuongeza kiasi cha nishati ya umeme kufikia zaidi ya Megawati 100.
Agizo hilo lilitolewa leo na Naibu
Waziri, Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani alipofanya
ziara yake katika kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya Gesi
cha Kinyerezi jijini Dar es Salaam,hii ni baada ya kuelezwa kuwa kituo
hicho kwa sasa kinazalisha 70 Megawati za umeme ambaohautoshelezi kwa
matumizi ya watanzania.
“Watanzania wamechoshwa na mgao wa
umeme na wanaimani kubwa na uzalishaji wa kituo hiki cha kuzalisha
umeme kwa kutumia gesi hivyo wanatarajia umeme wa uhakika katika kufanya
shughuli mbalimbali za uzalishaji na kujipatia kipato”,alisema
Dkt.Kalemani.
No comments:
Post a Comment