TTCL

EQUITY

Tuesday, December 15, 2015

MAWAZIRI WAPYA WAANZA KUINGIA VITUO VYAO VYA KAZI

mah1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira na Muungano Mh. January Makamba akipokea nyaraka za Ofisi wakati akikabidhiwa Ofisi na Waziri aliyemaliza muda wake Dk. Binilith Mahenge Ofisini Mtaa wa Luthuli Dar es Salaam.
 
mah2
Naibu Waziri   Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira na Muungano Mh. Luhaga Mpina akikabidhiwa nyaraka za Ofisi na Naibu Waziri aliyemaliza muda wake Mh. Stephen Masele . Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini jijini Dar es Salaam
 
mah3
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais akiwa Bwana Sazi Salula akiwa katika picha ya pamoja na  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira na Muungano Mh. January Makamba na Waziri aliyemaliza muda wake Dkt. Binilith Mahenge mara baada ya makabidhiano ya Ofisi.

Waziri Mpya wa Ofisi ya Makamu wa Rais January Makamba akiwa na Naibu wake Mpina walipowasili ofisini leo.

Naibu Waziri, Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akiongea na watendaji wa Wizara na Taasisi alipokutana nao katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango.  Akizungumza na uongozi wa Wizara na Taasisi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji aliwaasa viongozi kutekeleza majukumu waliyokabidhiwa na kuhakikisha bajeti ya Serikali inalenga vipaumbele vinavyogusa wananchi katika kutekeleza ahadi ya Serikali.
Naibu Waziri, Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akijadiliana na watendaji wa Wizara na Taasisi kuhusu masuala mbalimbali ya Wizara pamoja na Taasisi zilizo chini ya Wizara.
 
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji kabla ya kuanza majadiliano na watendaji wa Wizara na Taasisi.
Waziri Mkuu Majaliwa akiwa na Waziri wa Ofisi yake Jenista.

si12
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Naibu Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde  wakati aliporipoti Ofisini kwake jijini Dar es salaam kuanza kazi Desemba 14, 2015. Katikati ni Waziri wa Nchi  Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenisa Mhagama .(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 
si13
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Naibu Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt Abdallah Possi   wakati aliporipoti Ofisini kwake jijini Dar es salaam kuanza kazi Desemba 14, 2015. Wapili kushoto  ni Waziri wa Nchi  Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenisa Mhagama  na kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 
si14
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama  (wapili kushoto), na Naibu Mawaziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Abdallah Possi  (wapili kulia)  na Anthony Mavunde (kulia) baada ya kuwakabidhi taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu wakati waliporipoti Ofisini kwa Waziri Mkuu kuanza kazi Desemba 14, 2015.
 
si15
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama (katikati), Naibu Mawaziri Dkt. Abdallah Possi (kulia) na Anthony Mavunde (wapili kulia)) baada ya mawaziri hao kuripoti  Ofisini kwake kuanza kazi Desemba 14, 2015. Kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt, Florence Turuka, Wanne kushoto ni katibu Mkuu Kazi na Ajira, Eric Shitindi na watatu kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Regina Kikula.

nap1
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiangalia moja ya kazi za wasanii katika kiwanda cha kutengenezea batiki alipotembelea ofisi za Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) leo hii jijini Dar es Salaam.
 
nap2
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi Lilian Beleko (kulia) akimkaribisha kwa furaha waziri wa Habari,Utamaduni na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye wizarani hapo leo hii jijini Dar es Salaam.
 
nap4
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye(kushoto) akiongea na menejimenti ya shirika la Utangazaji Tanzania-TBC(hawapo pichani) wakati alipotembelea makao makuu ya shirika hilo ili kujua changamoto walizonazo na jinsi gani atawasaidia kama waziri mwenye dhamana.
 
Naibu Waziri ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jaffo akishiriki zoezi la kuwapima uzito mmoja wa watoto waliokuwepo katika kituo cha Afya Bahi baada ya kufanya ziara ya kukagua utoaji Huduma za afya katika wilaya ya Bahi, Mkoani Dodoma.
 
Naibu waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jaffo akizungumza na wagonjwa Mara baada ya kukagua wodi ya akina mama katika Kituo cha afya bahi.

No comments:

Post a Comment