Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick |
Hayo
yamesemwa leo na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadick,
wakati akipokea vifaa vya usafi na dawa za kuzuia magonjwa ya kuambukiza
hususani Kipindupindu vyenye thamani ya Milion 15.
Amesema watendaji wengi wameshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo
kwa kubebana na watumishi wao na kushindwa kutekeleza majukumu yao
ipasavyo kwa kuwasingizia wanasiasa wanawaingilia katika utekelezaji wa
majukumu yao.
Meck Sadiki amewataka watendaji hao kutokubali kuingiliwa katika
majukumu yao na wasimamie sheria ya kazi zao zinavyowataka na kuacha
kuwalea watumishi wazembe.
Kwa upande wao wadau wa maendeleo nchini wameiomba serikali kuhakikisha inasimamia vitendea kazi vinavyotolewa na wahisani.
No comments:
Post a Comment