Wakulima wa mikoa ya Lindi na Mtwara wameshauriwa
kutumia teknolojia ya mifuko ya PICS inayotumika kuhifadhia mazao, kama
njia bora ya kuyakinga ili yasiharibiwe na wadudu na kuachana na
kutumia njia ya kemikali ambayo inaweza kuleta athari baadae.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Fatma Salum Ally
Akizungumza
mkoani Mtwara katika semina ya kuwajengea uwezo wadaau wa kilimo juu ya
matumizi ya teknolojia hiyo, mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally,
amesema wakulima wengi hapa nchini wanakumbwa na changamoto ya upotevu
wa mazao baada ya mavuno, na ndio wanaoathirika kwa kiasi kikubwa
ukilinganisha na serikali.
Aidha, amesema uwepo wa mifuko hiyo umetokana na kuwepo kwa wadudu
waharibifu wanaoshambulia mazao ghalani hasa Dumuzi ambao uharibu mazao
ya wakulima masikini katika nchi zinazoendelea, na kuwakwamisha wakulima
wanaotegemea mazao hayo kwa chakula na biashara ili kuongeza kipato
katika kaya zao.
Kwa upande wake, mshauri mwelekezi wa mradi huo ambao ulianza kufanya
kazi mwaka 2014, Bernadetha Majebele, amesema mradi huo una malengo
kadhaa kwa wakulima ikiwa ni pamoja na kuwafanya wakulima wadogo kujua
namna ya kuhifadhi chakula chao na kukitumia baadae, na kuwatoa
watanzania katika matumizi ya kemikali katika kuhifadhi mazo kwasababu
ina athari kiafya.
No comments:
Post a Comment