Wakulima
zaidi ya 300 waliopo katika vijiji vya Kibanda, Semngano na Mkinga
wilayani Muheza wamekataa kuondoka katika mashamba yao yenye mazao ya
kudumu kufuatia watendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo kwenda kuyapima
na kuweka mawe ya mipaka kisha kuwaamuru kuachia mashamba hayo kabla
nguvu ya dola haijatumika dhidi yao.
Wakizungumza katika mashamba hayo, baadhi ya wakulima wameiomba
serikali kuharakisha kutatua migogoro ya ardhi ikiwemo ya wakazi wa
Muheza inayosababishwa na baadhi ya watumishi wake hatua ambayo
imechangia sehemu kubwa ya wanacnhi kuichukia serikali yao kwa sababu ya
watu wachache.
Wakifafanua jinsi walivyopata mashamba hayo baadhi ya wakulima
wakiwemo wazee wamesema wameanza kulima tangu mwaka 1983 chini ya
operesheni nguvu kazi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la rais wa kwanza
hayati Baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere la kuwataka
wapande mazao ya kudumu ili waweze kujitosheleza kwa chakula.
Kufuatia hatua hiyo mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Muheza
Bwana Adrian Jungu akielezea sakata hilo amesema awali shamba hilo lenye
ukubwa wa hekari 454 lilikuwa likimiliwa na mfanyabiashara mwenye asili
ya kiasia lakini baadae halmashauri walilitaifisha shamba hilo baada ya
mwekezaji kuondoka nchini.
No comments:
Post a Comment