Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa (kushoto) akilakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), Felix Ngamlagosi alipofanya ziara ya kujua utendaji wa mamlaka hiyo, Dar es Salaam.
Akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi na viongozi wa
Ewura, Profesa Mbarawa ameagiza mamlaka hiyo, kufungua haraka matawi
katika Kanda mbalimbali nchini ili kurahisisha uboreshaji wa huduma za
maji.
Pia ameitaka Ewura, kutoa adhabu kali kwa taasisi, mamlaka za maji na wafanyabishara wa maji wanaotoa huduma zisizoridhisha hasa kuuza maji machafu.
Waziri Profesa Mbarawa, ameuagiza uongozi wa Ewura, kumpelekea mikataba ya utendaji ya Mwenyekiti wa Bodi na Mkurugenzi Mkuu, ili kila mmoja afuatiliwe uwajibikaji wake.
Waziri, Profesa Mbarawa ambaye katika ziara hiyo alifuatana na Naibu wa Wizara hiyo, Injinia Isack Kamwela, amesifia utendaji mzuri wa mamlaka hiyo.

No comments:
Post a Comment