Diamond Platnumz na Wema Sepetu wameendelea kuliimarisha penzi lao kadri
siku zinavyoenda. Uhakika wa kuwa wapenzi hawa wenye uhusiano wa ‘on
and off’ wamerudiana kwa kasi, ulijulikana baada
ya picha zao wakiwa
Hong Kong kusambaa mtandaoni hali iliyopelekea kuzuka mgogoro mkubwa
kati ya Diamond na mpenzi wake Penny ambaye kuna tetesi kuwa
wameshaachana rasmi.
Hii ilikuwa jana pale Leaders club kwenye show ya Diamond ambapo
Wema Sepetu alipanda kwenye stage na kuongea na mashabiki waliofika
kwenye show hiyo.
Kwenye hiyo show Diamond aliuliza,”Mnataka kumjua mchumba wangu”?
Show ilivyoendelea Diamond alitaka kuimba wimbo wa ukimwona akasema,
“Naskia ninayetaka kumuimbia wimbo huu yupo humuhumu ndani”.
Wema Sepetu akapanda kwenye stage wakaimba na kucheza wote.
No comments:
Post a Comment