Abiria wanaosafiri na basi la Super Shem kutoka
jijini Mbeya kwenda katika jiji la Mwanza wameamua kufunga barabara eneo
la Ilonga wilayani Mbarali mkoani Mbeya, baada ya gari hilo kupata
itilafu na kushindwa kuendelea na safari.
Tatizo hilo limetokea katika eneo hilo majira ya saa moja kasoro na kuahidiwa kutatuliwa tatizo hilo kwa kupewa basi jingine ndani ya masaa matatu, lakini hadi majira ya saa sita mchana hakuna dalili zozote zilizoonyesha kupata usafiri mwingine kuelekea jijini Mwanza.
Kutokana na ahadi hiyo hewa,wasafiri wakafanya jitihada za kuwasiliana na jeshi la polisi na SUMATRA ili kuweza kupata namna nyingine ya kusafiri lakini muda ukazidi kwenda bila mafanikio ndipo wakaungana kwa pamoja na kuamua kufunga barabara kwa lengo la kutatuliwa kero hiyo.
''Tumefanya kila namna ili kuweza kupata msaada ikiwa ni pamoja na kuongea na SUMATRA pamoja na jeshi la polisi lakini tumeahidiwa kupewa basi jingine hadi wakati huu hatujui hatima yetu ikoje ndiyo maana tumefunga barabara”alisikika abiria ambaye jina lake halikufahamika mara moja.
Hata hivyo abiria wengi wanawake hasa waliobeba watoto wadogo wameonyesha kukerwa na kero hiyo kutopata ufumbuzi wa haraka wakati wao wamebeba watoto wadogo na eneo hilo halina huduma zozote za kijamii kama chakula, maji na vyoo vya kujisaidia.
''Hapa tulipo tumebeba watoto wadogo na wengine wanawahi kwenye shughuli mbalimbali kutudanganya kama watoto sii jambo zuri hata kidogo,tunawaomba wahusiika waingilie kati tupate kusafiri salama''
Hata hivyo Kamanda wa polisi mkoani Mbeya ACP Ahmed Msangi amesema kuwa amepata taarifa za tukio hilo na ametuma vijana wake kuelekea katika eneo hilo ili kuongeza ulinzi wakati wakifanya utaratibu wa kupata namna ya usafiri mwingine wa abiria hao.
No comments:
Post a Comment