TTCL

EQUITY

Friday, December 4, 2015

Vituo vya afya vyakabiliwa na upungufu wa ARV

Baadhi ya vituo vya afya nchini vinakabiliwa na upungufu wa dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI kwa watoto waliokwisha anza kutumia dawa hizo na kunasababisha watoto kutopata dozi sahihi na kwa wakati kunakopelekea watoto kupatwa na usugu

Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI nchini Tanzania Dkt. Fatma Mrisho
Hayo yamebainishwa na wahudumu wa tiba katika kituo cha afya cha Madibila Wilayani Mbarali baada ya waratibu wa UKIMWI mkoa wa Mbeya kutembelea hospitalini hapo.
Dr Edwin Mweleka ambaye ni mratibu wa mkoa tume ya kudhibiti ukimwi (TACAIDS) amekiri kuwepo kwa upungufu huo huku akiongeza kuwa tayari mipango ya makusudi ya kutatua tatizo hilo imeanza.
Aidha kutokana na mpango huo pia Dr Mweleka amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa hatua ya kufuta sherehe za maadhimisho ya siku ya UKIMWI badala yake fedha za sherehe hizo kuelekezwa kununulia dawa.
Naye afisa maendeleo ya jamii mkoa wa Mbeya Stella Kategile amewataka wazazi na walezi kutekeleza wajibu wao licha ya kuegemea katika majukumu ya shughuli za kiuchumi na kutozingatia watoto.

No comments:

Post a Comment