TTCL

EQUITY

Friday, December 4, 2015

Hakuna aliyenichangia kuingia ikulu - Magufuli

Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli, amesema hakuna mfanyabiashara yeyote aliyemchangia kumuwezesha kuingia Ikulu katika kampeni za uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu. "Nilijiepusha na fedha au mchango wowote kutoka kwa wafanyabiashara, na kama yupo mfanyabiashara yeyote ambaye  alinichangia hata shilingi mbili asimame hapa aseme, nilikwepa kwa sababu nilitaka iwe KAZI TU,"alisema jana wakati akiongea na viongozi wa sekta binafsi nchini.
Alisema wakati wa kampeni hadi kufikia siku ya uchaguzi mkuu Oktoba 25, mwaka huu, hakupokea senti yoyote kutoka kwa wafanyabiashara kwa kuwa alijua akiingia madarakani anakwenda kufanya kazi tu.
Dk. Magufuli alitoa kauli hiyo jana Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na wafanyabiashara na wawekezaji wa sekta binafsi, katika kikao cha pamoja kilichoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Baraza la Biashara la Taifa (TNBC) kwa ajili ya kufahamiana.
Akizungumza katika mkutano kati yake na wafanyabiashara nchini Dkt. Magufuli amewataka wafanyabiashara kuweka maslahi ya taifa mbele katika shughuli mbalimbali za maendeleo na kuiwezesha nchi kuondokana na umasikini...


Dkt. Magufuli amesema katika siku hizo saba endapo maagizo yake hayatatekelezwa basi sheria itafuata mkondo wake huku akiwataka wafanyabiashara kuwa wazalendo na taifa katika kulea maendeleo.
Kwa upande mwingine ametoa angalizo kwa watendaji wa serikali wenye tabia ya kuchelewesha maamuzi katika suala la uwekezaji bila sababu za msingi kuacha vitendo hivyo ili kutoa fursa kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.
Akizungumza katika mkutano huo mwenyekiti wa Sekta binafsi nchini Tanzania Dkt. Reginald Mengi ameitaka serikali kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji pamoja na kushughulikia rushwa ambayo inaonekana kushamiri na kufifisha ndoto ya Tanzania kuwa taifa lenye kipato cha kati kutoka cha chini.

No comments:

Post a Comment