TTCL

EQUITY

Friday, December 4, 2015

Halmashauri zatakiwa kusimamia sheria za usafi

Mkurugenzi Tawala za Mikoa nchini kutoka ofisi ya waziri mkuu nchini TAMISEMI Bi Suzane Chekani amezitaka kila halmashauri nchini kusimamia na kutumia sheria zake ndogo zinazosimamia maswala ya usafi zilizopo kwa kila manispaa.


Mkurugenzi Tawala za Mikoa nchini kutoka ofisi ya waziri mkuu nnchini TAMISEMI Bi Suzane Chekani
Bi. Chekani ameyasema hayo jana jijini Dar es salaam wakati alipofanya ziara ya kukagua usafi kwa manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es salaam na kuzitaka manispaa zote nchini kusimamia maswala ya usafi hasa maeneo ya chakula ambayo wameyakuta ni machafu.
Aidha Bi. Chekani ametaka kuwe na ushirikishwaji wa wadau mbalimbali wa maendeleo nchini ili kuongeza nguvu ya pamoja katika kupambana na matatizo ya magonjwa ya mlipuko ambayo imekuwa ni tishio kubwa kwa afya za watanzania kwa sasa.
Kwa upande wake mganga mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Grace Magembe amesema kuwa sheria za kutozwa faini kwa wale ambao wanachafua mazingira kwa makusudi kwani tayari wameweka faini ya shilingi 500.

No comments:

Post a Comment