WIZARA
ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, imefafanua kuwa
sifa ya kitaaluma ya waziri wa wizara hiyo ni.......... Profesa Joyce Ndalichako; na siyo Dk Joyce Ndalichako.
Taarifa
iliyotolewa jijini Dar es Salaam juzi na Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini cha wizara hiyo, ilisema tangu alipoteuliwa kushika wadhifa
huo wiki iliyopita, kwa bahati mbaya sifa ya kitaaluma ya waziri huyo,
imeendelea kujulikana kama Dokta.
“Tunapenda
kuufahamisha umma kwamba cheo cha kitaaluma cha Waziri wa Elimu,
Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Dokta Joyce Ndalichako kwa sasa
ni Profesa Joyce Ndalichako”, ilisisitiza taarifa hiyo ya wizara
Taarifa
hiyo ilisema wafanyakazi wa wizara hiyo, wanampongeza waziri kwa uteuzi
huo na wanaahidi kumpa ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake kwa
weledi na uadilifu katika kuendeleza sekta ya elimu na mafunzo nchini
No comments:
Post a Comment