TTCL

EQUITY

Wednesday, December 30, 2015

Ripoti uchunguzi unenepeshaji wa ng'ombe kutua kwa Waziri Mkuu leo

Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, leo inatarajia kuikabidhi ofisi ya Waziri Mkuu ripoti ya uchunguzi wa unenepeshaji wa ng’ombe kwa kutumia mbolea na kemikali.
Serikali kupitia wizara hiyo iliamua kufanya uchunguzi baada ya Nipashe kuchapisha ripoti iliyofichua kuwapo kwa baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu ambao hutumia kemikali zisizofaa katika kuwanenepesha wanyama hao kabla hawajafikishwa sokoni.
Imegundulika kuwa baadhi ya wafanyabiashara mkoani Shinyanga wamekuwa wakiwadunga sindano zenye dawa na kemikali za kuwanenepesha ndani ya muda mfupi ng’ombe wao sambamba na kuwalisha mbolea aina ya Urea ili kuwa na ng’ombe wenye madaraja ya juu na kujiingizia kipato kikubwa bila kujali afya za walaji wa kitoweo kitokanacho na wanyama hao. Baada ya taarifa hiyo kuchapishwa, wizara hiyo ilimtuma mtaalam wake kufanya uchunguzi ambapo kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo Tanzania, Dk.
Abdu Haughaimo, ripoti yake itakabidhiwa kwenye ofisi ya Waziri Mkuu leo.
“Uchunguzi wa awali unaonyesha ng’ombe hao walipewa dawa za kuzuia magonjwa ambazo ni minyoo, ndorobo, ukitaka kumnenepesha mnyama, kwanza unatakiwa kumpa dawa ya kumsafisha ili asipate vimelea vya maradhi,” alisema na kuongeza.
 
“Ripoti imejaa mambo mengi ambayo siwezi kukupa hadi tuikabidhi,” alisema.
Katika toleo lake Na. 0578704 la Desemba 21, mwaka huu, Nipashe ilieleza namna walaji wa nyama ya ng’ombe nchini walivyo katika hatari ya kupata maradhi ya saratani na kushindwa kufanya kazi kwa figo, ini na moyo kutokana na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu kutumia kemikali hatarishi kuwanenepesha wanyama hao kabla hawajafikishwa sokoni.

No comments:

Post a Comment