 |
Rais John Magufuli ameagiza siku ya Uhuru itumiwe kufanya usafi |
|
Rais
John Magufuli ameongoza kwa vitendo zoezi la kufanya usafi leo kama
alivyoelekeza baada ya kufuta shamrashamra za maadhimisho ya siku ya
Uhuru, Disemba 9.
Rais Magufuli na mkewe Janeth wamefanya usafi
katika maeneo ya Feri, eneo ambalo liko mita kadhaa kutoka Ikulu jijini
Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan,
aameshiriki kikamilifu na baadhi ya wananchi wakazi wa eneo lake la
Oysterbay- Karume Raod, kufanya usafi
ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama
alivyoagiza Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo
limefanyika nchini kote hii leo.
 |
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Pamoja na Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda
wakishiriki kuzoa taka na baadhi ya wananchi wa eneo Morocco, wakati wa
zoezi la kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya
miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe
Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika nchini kote hii leo. |
 |
Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete
wakifanya usafi katika soko kuu la Chalinze leo Desemba 9, 2015 ikiwa ni
kuadhimisha miaka 54 ya Uhuru |
Naye rais wa serikali ya awamu ya nne, Jakaya
Kikwete na mkewe Salma nao wameingia barabarani na kuungana na wananchi
kufanya usafi katika maeneo yao katika harakati za kutokomeza magojwa
yanayotokana na uchafu kama kipindupindu.
Aidha, Makamo wa rais,
Samia Suluhu yeye ameonekana akifanya usafi katika eneo la ufukwe wa
bahari wa ‘Coco Beach’ jijini Dar es Salaam huku Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa yeye ameingia katika eneo la Soko la Kariakoo kujiunga na zoezi
hilo.
 |
Wananchi wa Mkoa wa Dodoma wakitekeleza agizo la Mh. Rais Maguful, la kufanya ufafi |
Wananchi kwa ujumla nchini wameonekana kuitikia wito wa
kufanya usafi katika maeneo yao kwa hamasa kubwa hali inayoonesha kuwa
Tanzania itaweza kutokomeza magonjwa ya mlipuko yanayotokana na uchafu.
 |
Wananchi wa Jimbo la hai Mkoani kilimanjaro wakishirikiana na Mh. Mbunge Freman Mbowe katika zoezi la kufanya usafi |
 |
Baadhi ya wasichan warembo wakishiriki kuunga mkono agizo la Rais kwakufanya usafi katika Jiji la Dar es Salaam |
No comments:
Post a Comment