Serikali
imeliagiza Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro Kumkamata mara moja na
kumfikisha Mahakamaini Meneja wa Kiwanda cha Kukoboa kahawa cha
Tanganyika Coffee Curing Company LTD cha mjini Moshi Andrew Kleruu kwa
tuhuma za kuhusika na upotevu wa magunia 36 yenye uzito wa kilogramu
1764 za kahawa kutoka kwa wanaushirika wa chama cha G32 kilichopo
mkoani humo.
Agizo
la mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amos Makalla likielekezwa kukamatwa kwa
Meneja wa Kiwanda cha kukoboa Kahawa cha Tanganyika Coffee Curing
Company Ltd Andrew Kleruu akituhumiwa kuhusika na upotevu wa magunia 36
katika ukoboaji wa kahawa kwa msimu uliopita.
Pamoja
na Mambo mengine Makala ameagiza kuchunguzwa kwa madai ya mishahara ya
wafanyakazi kiwandani hapo yanayofikia kiasi cha shilingi milioni
77.pamoja na kodi inazodaiwa na mamlaka ya mapao nchini TRA mkoani
Kilimanjaro kiasi cha sh.milioni 390.
Kauli
ya Makala imenilazimu kuutafuta uongozi wa chama cha G32 ili kujua ni
namna gani hali hiyo imekuwa ikikatisha tamaa wakulima wa kahawa
kuendelea na kilimo cha zao hili.
Tuhuma
za ubadhirifu wa fedha zimeendelea kuukumba mkoa wa Kilimanjaro katika
miezi ya hiv karibuni huku watumishi wa idara mbalimbali wakihusishwa na
tuhuma hizo.
No comments:
Post a Comment