TTCL

EQUITY

Saturday, December 12, 2015

Mamlaka ya Mapato nchini TRA yapanga utaratibu wa kutoa bure mashine za EFD’S kwa wafanya biashara.

Kaimu kamishna mkuu wa  TRA Dr. Philiph Mpango
Mamlaka ya mapato Tanzania TRA inaangalia utaratibu wa kutoa bure  mashine za kutolea risiti za EFD’s kwa wafanyabiashara ili kurahisisha ukusanyaji wa kodi.

Kaimu kamishna mkuu wa  TRA Dr. Philiph Mpango amesema hayo wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari ambapo amesema mwisho wa watumishi wa mamlaka hiyo kujaza fomu za mali wanazomiliki ni  December 15 huku akiomba wananchi kusaidia kufichua vitendo vya ufisadi kweneye mamlaka hiyo.
Kuhusu  waliotorosha makontena bila kulipia ushuru  amesema  wafanyabiashara 13 tuu ndio wamemaliza kulipa kwa hiari katika muda uliotolewa na rais  na wengine 15 wamelipa sehemu na bado wanadaiwa na watalazimika kulipa  kwa mabavu ambapo kiasi kilichopatikana ni shilingi bilioni 10.

No comments:

Post a Comment