Rais Dakta JOHN MAGUFULI ameliapisha baraza la mawaziri alilolitangaza Alhamisi juma hili.
Baraza hilo la mawaziri na manaibu waziri lenye mawaziri kumi na
tisa ni dogo likilinganishwa na baraza la mawaziri lililopita lililokuwa
na mawaziri na manaibu mawaziri sitini.
Akitangaza baraza hilo mbele ya waandishi wa habari Ikulu jijini
Dar es salaam alisema baadhi ya wizara zitakuwa na manaibu waziri na
nyingine hazitakuwa nao.
Amesema lengo kubwa ni kuwa na baraza dogo la mawaziri linaloweza
kufanya kazi kwa ufanisi zaidi kama alivyoahidi wakati wa kampeni ya
uchaguzi kuwa ya kuwa na baraza dogo, ambalo litasaidia kupunguza
matumizi ya serikali.
Katika kutekeleza hilo, rais amefuta semina elekezi iliyopangwa na
Wizara ya Utumishi kwa mawaziri na manaibu waziri ambayo ingegharimu
shilingi bilioni mbili na kusisitiza kuwa fedha hizo zitapangiwa
matumizi mengine.
No comments:
Post a Comment