BLOGGER chipukizi nchini Dotto Mzava, amefariki Dunia katika ajali ya barabarani Desemba 14, 2015 Jijini Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Mwenyekiti wa Mtandao wa Bloggers Nchini, (TBN),
ambao marehemu alikuwa ni mwanachama wake, Bw. Joackim Mushi amesema
Dotto ambaye alikuwa akifanyia kazi Jamii Media (Wamiliki wa mtandao wa
Jamii Forum) amapo pia alikua akimiliki tovuti yake ya Fikra pevu, Marehemu amefariki kwa ajali ya pikipiki ingawa haikuelezwa ajali
hiyo imetokea maeneo gani hasa ya jiji la Dar es Salaam.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jina lake Lihimidiwe Amin.
No comments:
Post a Comment