MWIGIZAJI mahiri Bongo, Wastara Juma Issa Abeid ‘Wastara’ amesema
suala la kuolewa tena halikwepeki licha ya kutokuwa na mawazo juu ya
suala hilo kwa sasa.
Akizungumza na paparazi wetu, Wastara ambaye ni nadra sana kukosea
awapo mbele ya kamera, alisema yeye kama mwanamke aliyekamilika hadhani
kama atakaa bila mwanaume lazima ataolewa tena.
“Mimi ni mwanamke niliyekamilika, suala la kuolewa ni lazima, japo
kwa sasa sifikirii kufanya hivyo, lakini sidhani kama nitaweza kukaa
bila mwanaume, lakini pia usumbufu kutoka kwao unaendelea,” alisema
Wastara
No comments:
Post a Comment