TTCL

EQUITY

Sunday, December 13, 2015

Afrika yakabiliwa na uhifadhi wa miyonzi

Nchi za Afrika ikiwemo Tanzania zinakabiliwa na changamoto kubwa ya uwezo mdogo wa kubaini na kuhifadhi mabaki ya mionzi inayoweza kuleta athari kwa binadamu na viumbe wengine, tatizo linalochangiwa na ukosefu wa vifaa vya kisasa na teknolojia.
Mkurugenzi wa idara ya mionzi kutoka tume ya taifa ya nguvu za atomic nchini Dkt. Mwizaruba Nyaruba.
 
Akizungumzia ukubwa wa tatizo hilo jijini Arusha mtaalam kutoka shirika la nguvu za Atomic duniani Bw. John Jonas amesema pamoja na tatizo hilo kuzikabili nchi nyingi duniani, ni kubwa zaidi kwa nchi maskini na kwamba hatua za kuzisaidia zinaendelea.

Akizungumzia hali hiyo baada ya wataalam hao kukutana na wadau wa technolojia ya mionzi kutoka nchi za Afrika mashariki Jijini Arusha mwakilishi wa tume ya nguvu za atomic kutoka Kenya Bw.Pius Masai Mwachi ameshauri nchi za EAC, kuangalia uwezekano wa kushirikiana pamoja kukabiliana na changamoto hiyo .

Kwa upande wake mkurugenzi wa idara ya mionzi kutoka tume ya taifa ya nguvu za atomic nchini Dkt. Mwizaruba Nyaruba amesema pamoja na changamoto zilizopo wanaendelea kubaini, kukusanya na kuhifadhi mabaki ya mionzi katika maeneo mbalimbali sambamba na kutoa elimu kwa umma juu ya madhara ya mabaki hayo .

No comments:

Post a Comment