Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
Wanachama wa chama hicho waliingia katika sintofahamu baada ya
diwani wa chama hicho kutoka Jimbo la Lupembe kupewa kiti maalumu katika
Jimbo la Njombe Kusini.
Akitoa ufafanuzi wa jambo hilo ambalo limeleta taharuki na
kulalamikiwa na baadhi ya wanachama wa Chadema, Mwenyekiti wa chama
hicho mkoa wa Njombe, Alatanga Nyagawa, alisema chama hicho kimeingia
katika mvutano kuhusiana na suala hilo na kuwaomba wanachama kuwa na
utulivu wakati likishughulikiwa.
Alisema jambo hilo huenda lilifanyika ngazi ya taifa idara ya
wanawake ya chama hicho, kwa kuwa majina yote yalipelekwa huko na
uchambuzi ulifanyika na kutumwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec).
Alisema kama kosa hilo alikufanyika katika chama ngazi ya taifa, litakuwa limefanyika Nec ambako majina hayo yalitumwa.
Nyagawa alisema jambo hilo linaweza kufanywa na chama chochote, kwani limetokea kwa bahati mbaya.
Aliwaomba wafuasi wa chama hicho kuwa watulivu wakati suala hilo
linashughulikiwa na uamuzi utatolewa na kwamba ikibainika kuna kosa
limefanyika, huenda akanyang'anywa udiwani na kupewa mtu wa chama hicho
Jimbo la Njombe Kusini.
Diwani huyo alipata shida wakati wa kuapa kutokana na kuwa na
wasiwasi na kushindwa kutamka kile kilicho kuwa kimeandikwa katika
karatasi ya kiapo.
No comments:
Post a Comment