TTCL

EQUITY

Tuesday, December 1, 2015

BARAZA LA MAWAZIRI LA MAGUFULI NI HATARI

Rais wa Tanzania, John Magufuli akiwa ofisini kwake Ikulu
Rais wa Tanzania, John Magufuli akiwa ofisini kwake Ikulu
KUSUASUA, kwa Rais John Magufuli, kutangaza Baraza la Mawaziri kunatokana na msimamo wake wa kuwachambua watu anaotarajia kuteua katika nafasi hiyo huku akiaandaa mikataba ya makubaliano itakayokuwa mwongozo kwa mawaziri hao.
Nia ya Rais, hadi kufikia hatua hiyo imetafsiriwa kwamba anataka kupata mawaziri ambao wataweza kwenda sambamba na kasi yake pamoja na wawajimbikaji.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinaeleza kwamba kwa sasa Rais Magufuli, anasuasua kutangaza baraza lake kutokana na kile kinachodaiwa ni kuandaa mikataba ambayo mawaziri baada ya kuteuliwa watalazimika kuisoma kwa muda wa siku mbili kabla ya kukubali uteuzi huo.
Chanzo hicho, kilieleza kwamba wale watakaokubali itabidi wasaini mkataba huo ili kukukabiliana na matakwa mkataba huo.
“Kwa sasa huyu jamaa anaandaa mikataba kwa ajili ya kuwapatia Mawaziri na Manaibu wake na wanatakiwa kuisoma ndani ya siku mbili na yeyote atakayekubaliana na mkataba huyo atalazimika kuisaini.
“Mikataba ya Mawaziri na Manaibu inalenga kuwabana watumishi hao na kukubaliana kuwa iwapo itatokea tatizo katika wizara husika wao watakuwa wa kwanza kuwajibishwa.
“Mkataba unalenga kuwafanya Mawaziri hao na Manaibu wao kuhakikisha wanafanya kazi kwa uaminifu, uadilifu, na kwa kujali maslahi ya jamii,” kilisema chanzo hicho.
Pia kilisema mkataba huo unaonekana unamasharti kwamba endapo siku mawaziri hao watajiingiza kwenye vitendo vya kifisadi au Wizara husika kulaumiwa watalazimika kujiuzulu bila kubembelezwa huku mhusika akifishwa kwenye vyombo vya sheria bila mjadala.
Aidha, chanzo hicho kiliongeza kuwa kwa sasa wabunge waliowengi wanaogopa nafasi za uwaziri na unaibu kwa madai kuwa kasi ya Rais Magufuli ni kubwa na inaweza kumtia hatiani mtumishi wakati wowote.
“Wabunge hao wanapata homa kubwa kutokana na hatua ya Rais Magufuli na Waziri Mkuu Majaliwa kuonesha ushujaa wa ajabu kwa kuwashambulia vigogo ambao wameshindikana katika vitendo vya ukwepa wa ulipaji kodi au kufanya ubadhilifu katika maeneo mbalimbali ikiwemo bandari.
“Kitendo kinachofanywa na Rais Magufuli ni sawa na kumvua nguo Kikwete (Rais Mstaafu Jakaya Kikwete) kwani kwa madudu ambayo yanaonekana inaonesha wazi kuwa nchi haikuwa na kiongozi na kama ilikuwa na kiongozi basi kiongozi huyo alikuwa na mkono wake.
“Sikiliza kijana haiwezekani nchi ikawa na wafanyabiashara wakubwa na matajiri wakubwa wanaokwepa kodi huku kiongozi wa nchi kwa kujua ama kutokujua anakaa nao meza moja kwa kuwapongeza kwa misaada kiduchu wanayotoa katika jamii huku wafanya biashara hao wakiongeza wigo waliyonacho na wasiyonacho jambo ambalo ni hatari,” kilisema.
Wakati huo huo kuna tetesi kuwa kutokana na kasi ya Rais Magufuli kwa sasa ndani ya CCM kuna mvutano mkubwa ambapo wanataka kubadilisha katiba ya chama hicho.
Mgongano uliopo kwa sasa ndani ya Chama ni kutaka kubadilisha katiba ya chama hicho ili rais asiwe mwenyekiti wa chama.
“Hofu hiyo inatokana na kasi ya Rais Magufuli na inasemekana akiwa mwenyekiti watendaji wote ambao wapo maofisini kihasara hasara watakuwa na wakati mgumu zaidi.
“Mbali na hilo kwa sasa inaonesha wale watu ambao walikuwa walikuwa wanapatiwa madaraka kwa njia ya kulindana itakuwa hadithi kwani waliowengi wanaweza kutimliwa,” kilisema chanzo hicho.
“Hata hivyo ndani ya CCM kuna makundi ambayo yanatamani Rais Magufuli kutoa agizo la kuchunguzwa kwa mali alizonazo mtoto wa Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Ridhiwan Kikwete.
“Kila mtu anajua kwamba mtoto huyo ana mali nyingi na anamiliki zaidi vituo vya mafuta na magari kibao sasa watu wanajiuliza mali hizo amezipata wapi?
“Lakini hapa kuna jambo zito ambalo linaweza kuwa na manufaa kwa upande wa upinzani kama kwa muda mfupi Rais Magufuli ameweza kufanya mambo makubwa na kubaini madudu mengi inakuwaje kwa rais aliyepita kwa maana nyingine hiyo inaweza kuwapa nguvu ya kumpeleka Kikwete (ICC),” kilisema chanzo hicho.

No comments:

Post a Comment