WANANCHI katika majimbo ya Arusha Mjini na Handeni Mjini, watafanya
uchaguzi wa wabunge wao kesho. Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC), Jaji Damian Lubuva, alisema hayo jijini Dar es Salaam jana.
Pia alisema wananchi wa Kata ya Mvomero mkoani Morogoro, nao
watamchagua diwani. Wananchi wa maeneo hayo, hawakupiga kura katika
uchaguzi mkuu, uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu.
Siku hiyo, uchaguzi uliahirishwa katika majimbo saba, ikiwemo Arusha
Mjini na Handeni Mjini, kata ya Mvomero na nyinginezo 34 nchini. Tangu
wakati huo, uchaguzi umeshafanyika katika baadhi ya majimbo na kata.
Lubuva aliwaomba wananchi waliojiandikisha kama wapigakura katika
majimbo na kata husika, kujitokeza kesho kwenye vituo walikojiandikisha
ili kuweza kupiga kura na kuwachagua na viongozi wanaowataka.
No comments:
Post a Comment