Msanii Mb Dog anatarajia kufanya kazi na msanii
mkubwa wa hip hop kutoka Marekani Lil Wayne, mara baada ya makubaliano
kukamilika.
Mb
Dog ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo
kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kuwa meneja wake yupo
safarini, na moja ya jambo atalofanya ni kuongea na Lil Wayne ili kuweza
kufanya nae kazi.
“QS Mhando yuko safarini, anafanya maongezi na Lil Wayne, tunasubiri
kupata clip kidogo tuwaletee, unajua mwenye mawazo madogo wanawaza
hivyo, kwa sababu Lil Wayne mtu tu kati ya watu”, alisema Mb Dog.
Pamoja na hayo Mb Dog amesema yeye anapofanya colabo na wasanii
wanaofanya vizuri sasa hivi sio kama anatafuta njia ya kurudi, bali
anachanganya ladha na kutanua soko la kimataifa.
“Kushirikisha sio sababu ya kutoka, ni kuchanganya ladha kwa sababu
nilishatokaga, tena mwenyewe, kwa sasa hivi nategemea kushirikisha mtu
ili kutoka kimataifa”, alisema Mb Dog.
Pia Mb Dog amesema kazi ambayo anatarajia kuiachia hivi karibuni ni
moja ya kazi nzuri na bora ambayo hajawahi kuifanya kipindi cha nyuma.
Rapa Lil Wayne kutoka Marekani
No comments:
Post a Comment