TTCL

EQUITY

Tuesday, March 10, 2015

Jeshi la Polisi lalazimika kuwatawanya wananchi waliofunga barabara mkambarani,Morogoro.

Jeshi la Polisi limelazimika kuwatawanya wananchi kijiji cha Mkambarani Mikese wilayani Morogoro baada ya kufunga barabara ya Morogoro Dar es Salama kufuatia tukio la ajali ya gari ndogo aina ya Toyota mark ii kugonga wapanda pikipiki  na kusababisha kifo cha  mama mmoja mwalimu wa shule ya msingi Mkambarani.

Vurugugu hizo zimedumu kwa muda ambapo wananchi walipanga mawe barabarani na kuzuia magari yanayotumia barabara hiyo wakilalamikia kuchoshwa na matukio ya ajali za mara kwa mara katika eneo hilo wakiitaka serikali kuweka matuta.

 
Kufuatia vurugu hizo za wananchi, serikali ya kijiji na mkuu wa polisi wilaya Zuberi Chembela na wamelazimika kutuliza wananchi hao waliokuwa wakizungumza kwa jazba na kuwaahidi jeshi la polisi litaweka ulinzi katika eneo hilo kuzuia matukio ya ajali.
 
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Lenard Paul amesema chanzo cha tukio ni gari ndogo kugonga wapanda pikipiki Godwini Mbena na alikua amempakiza mkewe Judith Mbega mwalimu wa shule ya msingi Mkambarani ambaye alifariki dunia na mumewe amejeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro ambapo amesema jeshi  la polisi litawachukulia hatua wananchi waliohusika kufanya vurugu za kufunga barabara.

No comments:

Post a Comment