Muda wa kuhudumu wa
rais wa kisiwa cha Zanzibar umeongezwa baada ya matokeo ya uchaguzi wa
eneo hilo kufutiliwa mbali na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kufuatia
madai ya udanganyifu.
Muda wa Ali Mohammed Shein kuwa mamlakani ulitarajiwa kukamilika siku ya jumatatu.
Alikuwa
akitafuta kuchaguliwa kwa awamu nyengine kama mgombea wa chama cha
CCM,huku mpinzani wake wa karibu Seif Sharif Hamad akijitangaza mshindi
wa shughuli hiyo iliofanyika tarehe 25 mwezi Octoba.
Rais anayeondoka madarakani amesema kuwa ataingilia kati ili kutafuta suluhu ya amani.
Wikendi iliopita ,mabomu mawili yalilipuka katika kisiwa cha Zanzibar,licha ya kuwa hakuna majeraha yalioripotiwa.
Uchaguzi uliopita kisiwani humo,ambamo ni kikuvutio kikuu cha Utalii umekumbwa na ghasia.
Waandishi wanasema kuwa kuna wanajeshi wengi katika eneo hilo.
Bwana
Hamad,mgombea wa upinzani kupitia chama cha UKAWA amewataka wafuasi
wake kuwa watulivu na kufanya amani siku ya jumatatu huku juhudi za
kidiplomasia zikiendelea kulingana na chombo cha habari cha AFP.
No comments:
Post a Comment