Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameamua na ameitangaza kesho,
Alhamisi, Novemba 5, mwaka huu, 2015, kuwa Sikukuu na siku ya mapumziko.
Rais Kikwete amefanya uamuzi huo, ili kuwawezesha Watanzania
kushiriki katika sherehe za kuhitimisha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya
Nne na kuingizwa madarakani Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam leo Jumatano, Novemba
4, 2015 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Yohana
Sefue, Rais Kikwete ametoa uamuzi huo kwa mujibu wa mamlaka aliyo nayo
chini ya Kifungu cha 3 cha Sheria ya Sikukuu za Kitaifa.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
4 Novemba, 2015
No comments:
Post a Comment