Watu kadha
wanahofiwa kufariki baada ya ndege iliyotengenezewa Urusi kuanguka muda
mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Juba, Sudan Kusini.
Ripoti zinasema huenda watu 40 wamefariki, baadhi wakiwa watu walioangukiwa na ndege hiyo ya kubeba mizigo ardhini.
Ndege
hiyo, iliyokuwa safarini kuelekea mji wa Paloch katika jimbo la Upper
Nile ilianguka kwenye ukingo wa mashariki wa Mto Nile.
Maafisa bado wanatafuta manusura.
Msemaji
wa rais wa Sudan Kusini Ateny Wek Ateny ameambia shirika la habari la
Reuters kwamba mhudumu mmoja wa ndege hiyo pamoja na mtoto, ambao
walikuwa kwenye ndege hiyo, wamenusurika.
Ubalozi wa Urusi nchini Uganda, ambao pia husimamia
Sudan Kusini, umesema unawasiliana na maafisa wa serikali Juba kupata
habari zaidi, kwa mujibu wa msemaji wake Radmir Gainanov.
Ajali hiyo imetokea siku chache tu baada ya ndege nyingine ya Urusi
kuanguka eneo la Sinai, Misri Jumamosi.
No comments:
Post a Comment