Mhubiri mashuhuri
kutoka Nigeria TB Joshua ni miongoni mwa wageni mashuhuri
watakaohudhuria sherehe ya kumuapisha John Pombe Magufuli kuwa rais mpya
wa Tanzania Alhamisi.
Bw Joshua ambaye ni mhubiri wa kanisa la Church of All Nations aliwasili jijini Dar es Salaam Jumanne.
Baada
ya kuwasili kwa mhubiri huyo, Bw Magufuli aliandika kwenye Twitter:
"Tumushukuru Mungu, tumepata ugeni wa Nabii TB Joshua, atashiriki nasi
katika sherehe nitakapoapishwa kuwa Rais wa awamu ya Tano wa Tanzania."
Baadaye, alikutana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika ikulu ya Nairobi.
Kiongozi
wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, ambaye ni rafiki wa karibu wa Bw
Magufuli, pia anatarajiwa kuhudhuria sherehe hiyo.
Tayari
muungano wa Cord unaoongozwa na Bw Odinga umeahirisha shughuli ya
kuwasilisha sahihi za kuunga mkono marekebisho ya katiba kwa Tume ya
Uchaguzi ya Kenya (IEBC) ili kuhudhuria sherehe hiyo.
Muungano huo ulikuwa awali umepanga kuwasilisha sahihi hizo leo.
Bw
Magufuli, aliyekuwa mgombea wa chama tawala cha CCM ataapishwa kuwa
rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada yake
kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Novemba 25, matokeo
ambayo yalipingwa na chama kikuu cha upinzani nchini humo Chadema.
Mgombea
urais kwa tiketi ya chama cha Chadema Edward Lowaasa aliibuka wa pili,
kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment