Mji mmoja kaskazini mwa Iceland umekuwa kipeperusha bendera ya taifa nusu mlingoti kila mkazi wa mji huo anapofariki.
Lakini sasa, madiwani wa mji huo wa Husavik wenye wakazi 2,000 wameamua kusitisha utamaduni huo.
Wanasema
utamaduni huo sasa haufai kwa sababu wakazi hawajuani kama ilivyokuwa
zamani, na si lazima wakazi wawe wanamfahamu aliyefariki, haya kwa
mujibu wa gazeti la Morgunbladid.
Husavik huvutia sana watu
wanaofika kutazama nyangumi na diwani mmoja kutoka eneo hilo Hjalmar
Bogi Haflidason anasema kupeperushwa kwa bendera nusu mlingoti huwa
kunashangaza watalii.
“Wengi huwa wanadhani kiongozi wa nchi amefariki,” anasema.
Uamuzi
huo haukupitishwa kwa kauli moja, na kumbukumbu za mkutano zilizopakiwa
mtandaoni zinaonyesha kuna madiwani kadha waliopinga mpango huo.
Mmoja
wao Sofia Helgasdottir aliambia tovuti ya Visir kuwa: "Huu ni utamaduni
ulioanza zamani na tumekua nao. Ninafikiri ni utamaduni mzuri sana.”
Kuhusu wageni kushangazwa, amesema wageni hao ndio wanaofaa kujifunza tamaduni za wenyeji.
No comments:
Post a Comment