Rais Ma Ying Jeou wa Taiwan (kushoto) na Rais Xi Jin Ping (kulia) |
Maafisa
nchini Taiwan wanasema kwamba rais wa nchi yao anatarajia kukutana na
rais wa China Xi Jin-ping nchini Singapore Jumamosi.
Itakuwa ni mara ya kwanza kwa marais wa nchi hizo mbili kukutana.
Wachambuzi wa mambo wanasema huu ndio mwanzo wa kufungua njia ya kufufua uhusiano baina ya nchi hizo mbili.
Rais wa Taiwan, Ma Ying-jeou, amesema lengo la mkutano huo ni kuimarisha amani katika eneo la Taiwan.
Ushirikiano wa nchi hizo umekua zaidi chini ya rais Ma wa chama cha KMT ambaye anaiunga mkono China.
China inaitazama Taiwan kama jimbo lililojitenga ambalo siku moja litarejea kuungana na upande na China.BBC
No comments:
Post a Comment