Unamkumbuka
yule dogo aliyeanzisha redio stesheni yake nyumbani kwao? Bila shaka
umewahi kusoma story yake kwenye kijarida cha kila mwezi kiitwacho
SHUJAAZ ambacho husambazwa na gazeti la Mwanaspoti na vibanda vya Coca
Cola. Sasa hivi, dogo ana habari mpya na njema kwa vijana na wote
wanaomfuatilia. Nyota imeanza kung’ara upande wake na sasa redio kubwa
Tanzania EAST AFRICA RADIO imeamua kumpa nafasi aweze kusikika hewani na
show yake mpya iitwayo SHUJAAZ.
“Show
yangu itahusika na lifestyle ya vijana kwa ujumla, bila kusahau burudani
kali, story za wana mbali mbali wanaojituma na kutoboa katika kufikia
malengo yao maishani. Pia, utawasikia vijana mbali mbali wakijadiliana
kuhusu ishu zinazowahusu, mfano PESA, MAPENZI, KAZI, MICHEZO,
UJASIRIAMALI n.k, ni lazima tupeane mashavu kama vijana.” Alisema DJ
Tee.
Show hiyo
itakayoanza rasmi JUMAMOSI hii (07/11/2015) saa TISA alasiri,
inatarajiwa kuvuta hisia za vijana wengi hasa wajasiriamali kwa kuwa
itahusika na ishu zote ambazo zinawahusu vijana kama DJ TEE mwenyewe
alivyoelezea.
No comments:
Post a Comment