Dkt. John Magufuli Rais wa Tananzania na Bi. Samiah Suluhu Makamu wa Rais |
John Pombe Magufuli
sasa ndiye rais mpya wa taifa la Tanzania baada ya kuapishwa rasmi
kufuatia ushindi wake wa wingi wa kura katika uchaguzi mkuu uliopita.
Akiapishwa
katika hafla iliohudhuriwa na viongozi mbalimbali,wakiwemo marais
kutoka mataifa ya Afrika mashariki na kusini, Magufuli ameapa kutimiza
ahadi zote alizotoa wakati wa kampeni za uchaguzi.
Magufuli ambaye
sasa ni rais wa awamu ya tano nchini Tanzania vilevile amewataka
viongozi wa upinzani nchini humo kukubali kushindwa na kushirikiana naye
katika juhudi zake za kuimarisha maisha ya taifa hilo.
Amesema kuwa licha ya kwamba alipata changomoto kubwa kutoka kwa upinzani alioupata amepata funzo kubwa kutoka kwao.
''Nashukuru
wagombea wenzangu kwa kutupa changamoto,tumejifunza mengi kutoka
kwao,lakini pia wajue kwamba uchaguzi umekwisha na rais ni John Pombe
Magufuli'',alijigamba.
Awali aliyekuwa rais wa taifa hilo Jakaya Mrisho
Kikwete aliwasili katika uwanja wa sherehe hiyo mbele ya umati mkubwa wa
watu waliomkaribisha kwa vifijo na nderemo.
Kikwete aliuzunguka uwanja huo akiwapungia mkono wa kwaheri raia hao waliojaa uwanja huo.
Baadaye Bendera ya utawala wake ilishushwa huku rais mpya John Magufuli akiapishwa na makamu wake wa rais Samiah Suluhu Hassan.
No comments:
Post a Comment